Tuesday, September 15, 2009

Tuzo ya Burt kwa Fasihi ya Kiafrika.

italeta ushindani kwa watunzi wa vitabu

Na Shadark


MRADI wa vitabu vya watoto Tanzania (CBP) kwa mara nyingine tena umeandaa Tuzo ya uandishi wa fasihi ya kiafrika inayojulikana kama ‘Tuzo ya Burt’ inayolenga kuhamasisha uandishi wa vitabu vya watoto wenye umri wa miaka 12 hadi 18 .

Tuzo hiyo ambayo itakuwa na zawadi nono kwa wandishi wa fasihi ya kiingereza pia itakuwa na lengo laa kuwapata watunzi wa vitabu wenye umahili wa kuandika riwaya katika lugha ya kiingereza zenye kuamsha shauku na mapenzi ya kusoma.


Akizungumzia tuzi hiyo Katibu Mtendaji wa (CBP) Pili Dumea anasema kuwa shindano hilo ambalo ni la pili tangu kuasisiwa Mwaka juzi linadhaminiwa na Tasisi moja inayojulikana kama Canadian for Development through Education (CODE) kutoka nchini Kanada.

Anasema kuwa Mwaka jana walipokuwa wanazindua tuzo hii kwa mara ya kwanza ,Mwandishi maarufu wa vitabu vya kiingereza Dk.Martha Mvungi alinukuliwa akisema;

“tuzo hii imekuja wakati Muafaka ,imekuja wakati waandishi wengi wa fasihi kwa lugha ya kiingereza wamekata tama na wameacha kuandika ,kwa sababu vitabu vyetu haviuzwi kwasababu sasa kuna motisha wa kuandika tutaandika”
Dumea anasema washindi watakaoweza kuandika riwaya au hadithi nzuri watazawadiwa jumla ya shilingi za kitanzania milioni 24 ambapo mshindi wa kwanza atapata sh milioni 13,wa pili million 7 na watatu atapata milioni 4.

aidha kitabu kitakapochapishwa mtunzi na mchapaji watakuwa na uhakika wa kukiuza kutokana na kuchukuliwa vyote na mradi wa CPB kwa ajili ya kusambazwa shuleni na mtunzi atakuwa na uhakika wa asiliamia 10 ya mauzo.


Anasema kuwa safari hii shindano hilo limeboreshwa na litahusisha miswaada ya waandishi itakayopitishwa kwanza kwa wachapishaji ambapo hapo awali shindano hio lilikuwa linahusisha waandishi moja kwa moja waliokuwa wanapeleka miswada hiyo ofisi za CBP.


“Safari hii chapishaji ndiye ataleta kazi ya mwandishi kwetu baada ya wasomaji wao kuikagua na kuipitia kasha kuridhika nayo kuwa inafaa na hii itasaidia kupata miswaada iliyo bora zaidi mana itashirikisha watu wengi katika kuchagua miswaada mizuri.” Anasema Dumea

Aliongeza kuwa mwandishi anatakiwa kuandika hadithi au riwaya ya matukio yanayotokea sasa katika nchi yetu kwa lugha ya kiingereza,kitabu kinatakiwa kiwe na kurasa 75 mpaka 150, iwe imefuata mtiririko wa matukio.

Dumea anasema kazi hilo ipelekwe katika ofisi zao zilizopo Makumbusho nyuma ya Benki ya NBC kabla ya Marchi 26 mwaka 2010 saa 10 jioni,mshindi atatangazwa kwenye sherehe za Canada Day zikazofanyika julai Mwaka Kesho.


“baada ya washindi watatu kupatikana vitabu vya vitachapishwa kisha kusambasambazwa shule zote na maktaba za mikoa nchi nzima ili watoto wote waweze kupata vitabu hivyo na kuvisoma kwa lengo la kuongeza wigo wa lugha.”Anaseza Dumea


Anasema kuwa shindano hilo litasaidia kuinua waandishi wa vitabu kwa kiingereza nchini pia itasaidia kuwajengea watoto tabia ya kupenda kusoma vitabu kwa kuwa watanzania walio wengi hawapendi kusoma vitabu.

Dumea anasema kuwa watanzania wa sasa hawapendi kusoma vitabu kwasababu hawana utamaduni huo hata kwa wale ambao wanaonekana ni wasomi,.

“kwasasa taifa linakabiliwa na ugonjwa wa kutopenda kusoma, wasomi hawasomi vitabu na wasio wasomi hawana muda wa kusoma vitabu tunataka kuanza kuhamasisha utamaduni huo”anasema

Dumea anasema kuwa ‘Ni matarajio yetu kuwa watanzania wengi watanunua vitabu hivyo hapo vitakapochapishwa ,Bwana Trelease aliwahi kuandika katika kitabu chake cha Read Aloud Handbook kuwa;

“idadi ya wanasesere ndani ya nyumba si muhimu kuliko idadi ya maneno katika kichwa cha mtoto’ maana yake ni kwamba idadi ya maneno katika kichwa cha mtoto itajengwa na usomaji wa vitabu .

mara tabia ya kusoma inapokuwa imejengwa kwa mtoto ,njia zote za kupata maarifa hufunguliwa na kujisomea hakuwi kwa taabu tena bali ni shughuli ya kujifurahisha.

Dumea anasema Tuzo ya Burt inalenga katika kuboresha upatikanaji wa vitabu na kuboresha elimu katika ngazi ya sekondari ,ambapo mwanafuzani huhitaji kuwa na ujuzi katika lugha ya kiingereza ili aweze kumudu masomo yake.

“naamini kuwa kwa kuchangia katika uchapaji wa vitabu bora vya kubuni na vinavyovutia ,wasomaji wa Tanzania watahamasika kusoma”

Tuzo ya Burt kwa Fasihi ya Kiafrika.

italeta ushindani kwa watunzi wa vitabu

Na Shadark


MRADI wa vitabu vya watoto Tanzania (CBP) kwa mara nyingine tena umeandaa Tuzo ya uandishi wa fasihi ya kiafrika inayojulikana kama ‘Tuzo ya Burt’ inayolenga kuhamasisha uandishi wa vitabu vya watoto wenye umri wa miaka 12 hadi 18 .

Tuzo hiyo ambayo itakuwa na zawadi nono kwa wandishi wa fasihi ya kiingereza pia itakuwa na lengo laa kuwapata watunzi wa vitabu wenye umahili wa kuandika riwaya katika lugha ya kiingereza zenye kuamsha shauku na mapenzi ya kusoma.


Akizungumzia tuzi hiyo Katibu Mtendaji wa (CBP) Pili Dumea anasema kuwa shindano hilo ambalo ni la pili tangu kuasisiwa Mwaka juzi linadhaminiwa na Tasisi moja inayojulikana kama Canadian for Development through Education (CODE) kutoka nchini Kanada.

Anasema kuwa Mwaka jana walipokuwa wanazindua tuzo hii kwa mara ya kwanza ,Mwandishi maarufu wa vitabu vya kiingereza Dk.Martha Mvungi alinukuliwa akisema;

“tuzo hii imekuja wakati Muafaka ,imekuja wakati waandishi wengi wa fasihi kwa lugha ya kiingereza wamekata tama na wameacha kuandika ,kwa sababu vitabu vyetu haviuzwi kwasababu sasa kuna motisha wa kuandika tutaandika”
Dumea anasema washindi watakaoweza kuandika riwaya au hadithi nzuri watazawadiwa jumla ya shilingi za kitanzania milioni 24 ambapo mshindi wa kwanza atapata sh milioni 13,wa pili million 7 na watatu atapata milioni 4.

aidha kitabu kitakapochapishwa mtunzi na mchapaji watakuwa na uhakika wa kukiuza kutokana na kuchukuliwa vyote na mradi wa CPB kwa ajili ya kusambazwa shuleni na mtunzi atakuwa na uhakika wa asiliamia 10 ya mauzo.


Anasema kuwa safari hii shindano hilo limeboreshwa na litahusisha miswaada ya waandishi itakayopitishwa kwanza kwa wachapishaji ambapo hapo awali shindano hio lilikuwa linahusisha waandishi moja kwa moja waliokuwa wanapeleka miswada hiyo ofisi za CBP.


“Safari hii chapishaji ndiye ataleta kazi ya mwandishi kwetu baada ya wasomaji wao kuikagua na kuipitia kasha kuridhika nayo kuwa inafaa na hii itasaidia kupata miswaada iliyo bora zaidi mana itashirikisha watu wengi katika kuchagua miswaada mizuri.” Anasema Dumea

Aliongeza kuwa mwandishi anatakiwa kuandika hadithi au riwaya ya matukio yanayotokea sasa katika nchi yetu kwa lugha ya kiingereza,kitabu kinatakiwa kiwe na kurasa 75 mpaka 150, iwe imefuata mtiririko wa matukio.

Dumea anasema kazi hilo ipelekwe katika ofisi zao zilizopo Makumbusho nyuma ya Benki ya NBC kabla ya Marchi 26 mwaka 2010 saa 10 jioni,mshindi atatangazwa kwenye sherehe za Canada Day zikazofanyika julai Mwaka Kesho.


“baada ya washindi watatu kupatikana vitabu vya vitachapishwa kisha kusambasambazwa shule zote na maktaba za mikoa nchi nzima ili watoto wote waweze kupata vitabu hivyo na kuvisoma kwa lengo la kuongeza wigo wa lugha.”Anaseza Dumea


Anasema kuwa shindano hilo litasaidia kuinua waandishi wa vitabu kwa kiingereza nchini pia itasaidia kuwajengea watoto tabia ya kupenda kusoma vitabu kwa kuwa watanzania walio wengi hawapendi kusoma vitabu.

Dumea anasema kuwa watanzania wa sasa hawapendi kusoma vitabu kwasababu hawana utamaduni huo hata kwa wale ambao wanaonekana ni wasomi,.

“kwasasa taifa linakabiliwa na ugonjwa wa kutopenda kusoma, wasomi hawasomi vitabu na wasio wasomi hawana muda wa kusoma vitabu tunataka kuanza kuhamasisha utamaduni huo”anasema

Dumea anasema kuwa ‘Ni matarajio yetu kuwa watanzania wengi watanunua vitabu hivyo hapo vitakapochapishwa ,Bwana Trelease aliwahi kuandika katika kitabu chake cha Read Aloud Handbook kuwa;

“idadi ya wanasesere ndani ya nyumba si muhimu kuliko idadi ya maneno katika kichwa cha mtoto’ maana yake ni kwamba idadi ya maneno katika kichwa cha mtoto itajengwa na usomaji wa vitabu .

mara tabia ya kusoma inapokuwa imejengwa kwa mtoto ,njia zote za kupata maarifa hufunguliwa na kujisomea hakuwi kwa taabu tena bali ni shughuli ya kujifurahisha.

Dumea anasema Tuzo ya Burt inalenga katika kuboresha upatikanaji wa vitabu na kuboresha elimu katika ngazi ya sekondari ,ambapo mwanafuzani huhitaji kuwa na ujuzi katika lugha ya kiingereza ili aweze kumudu masomo yake.

“naamini kuwa kwa kuchangia katika uchapaji wa vitabu bora vya kubuni na vinavyovutia ,wasomaji wa Tanzania watahamasika kusoma”

Monday, June 22, 2009

Grumet Reserve fund, kampuni iliyogeuka tishio Mkoa wa Mara.

*watoto wafungwa, mama zao wabakwa ,vijana wacharazwa bakora* wananchi wakosa amani * DC:wanajipeleka wenyewe ,Waziri :ni watoto wenu wenyewe wanaowatesa. *Mwekezaji wanavunja sheria za hifhadhi kimakusudi.
*Wananchi huu ni ukoloni mamboleo unaitwa uwekzaji,

Na mchambuzi wetu

UKITAKA kufahamu umhimu wa Sekta ya uwekezaji nenda mkoa wa Mara na ukitaka kufahamu uchungu wa sekta hiyo usikose kwenda katika mkoa huo kwani kila jema na baya la wawekezaji utajifunza huko.

Mkoa wa Mara ambao ungekuwa kielelezo kizuri cha kihistoria na mambo mabalimbali kutokana na mwasisi wa taifa hili hayati baba wa Taifa, Mwal.Julias Nyerere kutokea huko umegeuka kuwa ng’ome ya wawekezaji wanaotesa wananchi wake.

Mkoa huo kwa hivi sasa unao wawekezaji wawili wakubwa ambao kila mtu anayetaka kujifunza faida na hasara za uwekezaji ambao sasa unaokana kama ukoloni mambo leo anaweza kwenda kujifunza kwa makampuni haya ya wazungu.

kwanza ipo kampuni ya uchimbaji madini kutoka kanada, Barrick hiyo imewekeza katika mgodi wa dhahabu North Mara Tarime, yapo mabaya yake lakini kwa sehemu kubwa wakazi wa eneo hilo wameanza kuyaona matunda (siku nikipata nafasi nitaeleza).

Lakini kwa upande mwingine ipo kampuni ya mwekezaji mwingine John Paul inayoitwa Grumet Game Reserve and Fund inayomiliki vitalu vya uwindaji vya Ikolongo na eneo la wananchi lilokuwa ‘Open area’ kwa uwindaji wa kienyeji akapewa kinyemela (hapo ndipo matatizo yalipoanzia).

Pia kampuni hiyo ambayo awali iliingia nchini kwa ajili ya uwekezaji wa Hoteli ya kitalii kabla haijavutiwa na uwindaji inayo hoteli inayojulikana kwa jina la Sasakwa Logde.

Mwekezaji wa kumpuni hii pia ameanzisha jeshi ambalo amweligawanya katika sehemu kuu mbili, ‘platuni’ya village Skaut (VGS)ambao wanafanyaka kazi kama wapelelezi wake na lipo kundi la pili ambalo linafanya kazi ya kulinda mipaka yote ya kampuni hiyo.

Wananchi wa vijiji vinavyopakana na hifadhi ya Serengeti wanasema eneo analomiliki mwekezaji huyo kwa ajili ya shughuli za uwindaji, utalii wa kupiga picha lilikuwa mali yao kwa ajili ya kuwinda kila msimu lakini wajanja wachache wakampatia sasa amegeuka kuwa tishio kwao.

Nilipozungumza nao wananchi wa maeneo ya Bunda na Serengeti wanaoshi kandokando ya hifadhi hiyo wamesema kwamba wamechoka kuvumilia kunyanyaswa kwa muda mrefu sasa wanataka kuona serikali ikikomesha unyanyasaji huo kwa kuvunja makubaliano hayo.

Wananchi hao kutoka vijiji vya Kunzugu,Nyamatoke,Mihale, Mariwanda,Kihumbu na Hunyari wilayani Bunda pamoja na Nyichoka Isenye na Singisi wilayani Serengeti wanadai kuwa wamekuwa wakinyanyaswa na askari wa kampuni hiyo lakini , sauti zao zimekuwa haisikiki serikalini kuhusiana na kilio chao.

Diwani wa kata ya hunyari (CCM) Sumera Kiharata ni miongoni mwa wananchi wanaolalamikia kampuni hiyo kuwa mkataba wake umejaa utata jinsi ilivyopata eneo hilo ndio maana uhusiano wale umekuwa mbaya na wananchi wa ukanda huo.

Ukanda unaoelezwa kwa wilaya ya Bunda unaupana wa Kilomita takribani 10 kutoka kwenye mto Rubana unaotenganisha hifadhi hiyo pamoja na makazi ya watu upande wa kusini na kaskazini kuna safu Mlima balili hivyo wakazi wa eneo wanabaki kwenye kisehemu chembamba

Diwani huyo anasema kwamba eneo la hifadhi ambalo kampuni ya Grumeti Reserve imewekeza ni mali ya wananchi wa Bunda ambao walikuwa wametengewa na serikali kwa ajili ya uwindaji wa kienyeji lakini katika mazingira yaliyojaa utata mwekezaji huyo amepewa.

“ huyu mwekezaji kinachofanya atusumbue ni watanzania wenzetu ambao wapo wizarani na tatizo lake la kwanza ni kwamba mkataba wake ni utata jinsi alivyoupata bila wananchi kushirikishwa wakati eneo hilo lilikuwa ‘open area’ kwa ajili ya wananchi kuwinda”anasema Kiharata

Diwani huyo anasema kwamba kufuatia mwekezaji huyo kumilikishwa eneo hilo bila makubaliano ya wananchi amekuwa akiwazuia kunywesha mifugo yao katika mto huo ambao wamekuwa wakiutumiwa kwa miaka mingi kwa mahitaji mabalimbali yakiwemo ya nyumbani.

Hali hiyo imesababisha wananchi hao kupata shida pale wanapojikuta wameingia hapo kwani hukumbana na kipigo cha askari ambao hujichukulia sheria mikononi huku wakitozwa faini isiyojulikana inapokwenda.

Mwenyekiti wa kijiji cha Kihumbu, Kiteta Thomas akizungumza kwa niaba ya wananchi wale anasema kwamba askari wa Mwekezaji huyo wamekuwa wakiwachapa wananchi wa eneo hilo kinyume na sheria za nchi pamoja na kuwabaka akinamama wanaokwenda kuchota maji katika mto huo.

“kuhusu huyu Mwekezaji sioni faida yake kulingana na uwekezaji wake kwani kabla yake kulikuwa na mradi wa SRCP ,huu mradi ulihamasisha jamii juu ya uhifadhi wa mazingira na kutunza wanyama kama tunavyotunza Ng’ombe lakini wajanja wakauondoa na kumweka huyu”anasema Thomas

Mwenyekiti huyo anasema kwamba mradi huo ulipokuwepo wananchi wa eneo hilo walikuwa wanafaidika kwa kupata gawiwo la wanyama 32 kila msimu ambapo kila kijiji kilikuwa na kamati iliyokuwa inahusika kuwauzia wananchi nyamba hizo kwa bei nafuu halafu faida yake inakwenda kufanya maendeleo ya vijiji.

“wakati huo tuliunda kamati za uhifadhi zikiwa na walinzi waliokuwa wanakamata majangili na watu wakahamasika kulinda wanyama ,Grumet alipokuja Mwaka 2004 akazuia uwindaji akasema nitakuwa natoa Mil.1.8 kila kijiji kwa Mwaka jambo ambalo halitekelezeki kikamilifu”anasema Mwenyekiti huyo.

Viongozi hao wanasema kwamba Waziri wa Maliasili na Utalii alipoalikwa na kampuni hiyo kwenda kuzindua barabara ya vumbi wanayoiita ya kituko kulingana na ukarabati wake Disemba 12 Mwaka jana katika eneo hilo walimweleza kuwepo watu waliochapwa na wengine kubakwa lakini hakutaka kuthibisha hilo.

“tulimweleza Waziri Mwangunga kuwa huyu Mwekezaji anachapa wananchi hapa vijijini lakini yeye akatujibu kwa jeuri kwamba mlishasikia mtoto wa mzungu anachapa watu hapa kama sio watoto wenu wenyewe ”anasema Mwenyekiti wa kijiji hicho.

Wakati wananchi wakilalamikia kampuni hiyo na kufikia hatua ya kutaka serikali iondoe kwa upande wa viongozi wa serikali majibu yao ni tofauti, mkuu wa wilaya ya Bunda ,Luten mstaafu Chiku Galawa yeye anasema kwamba adhabu wayopata inatokana na wananchi wenyewe kuvunja sheria za hifadhi.

Luten Galawa anasema kuwa amebaini kwamba wananawake wengi wanaolalamikia kubakwa na askari wa Kapuni hiyo inatokana na wao wenyewe kujirembesha na kuwafuata askari hao porini.

“Tumepokea malalamiko hayo wengine wakilalamikia hata kubakwa lakini tulipofanya uchunguzi tukabaini kwamba vitendo vya kubawa vinaongezeka mwisho wa mwezi wanapojua kwamba askari hao wamekula mishahara ndipo akina mama hao hujirembesha na kuupara kisha wanakwenda huko”alisema Galawa

Alisema kwamba walishawazuia wanawake wasijirembeshe wakati wanakwenda kutafuta kuni kwani kufanya hivyo ni kuwavutia wanaume lakini wamekuwa wakipuuza na kuwafuata askari hao porini waume zao wakijua ndipo huanza kudai wamebakwa kitu ambacho hakina ukweli.

Nilipomuuliza kwamba anampango gani kuhakikisha anaunda hata kamati ya ujirani mwema itakayotumika kuwakutanisha wananchi na kampuni hiyo ili kuondoa uhasama uliojijenga kwenye kamii aling’akal;

“Sheria zipo lakini watu hawataki kuzifuata unataka tuwakutanishe ili waruhusiwe kwenda hifadhini au tukutane kufanya nini ni wajibu wa kila mwananchi kuzingatia sheria zilizokwishawekwa basi”anasema DC huyo.

Kiongozi mwingine anayebeza kilio cha wananchi ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bunda ………yeye anasema kwamba katika halmashauri yao wanaridhika mapato wanayoyapa ya Milion.4 kwa Mwaka pamoja na Mil.1.8 kila kijiji.

Mwenyekiti huyo anasema kama yapo malalamiko ya kunyanyaswa kwa kupigwa watu wanaopaswa kuyashughulikia na polisi wala sio mtu mwingine.

Kauli kama hizo ndio zimewachosha wananchi hao wakiwa wamenizunguka huku nyuso zao zikionyesha kuwa na shauku ya kunieleza jambo mhimu wakazi wa hunyari waliniambia kwamba malalamiko yao wa nataka niyafikishe kwa Rais Jakaya Kikwete au Kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda aweze kuwaokoa.

Wanasema kwamba wamejeribu kwenda hadi wizara ya maliasili na utalii kutaka Mwekezaji huyo aondolewe lakini wakajibiwa kuwa ni lazima wafuate utaratibu wa kukaa mikutano ya vijijini ili mihutasari ya mikutano ya hadhara iwasilishwe Halamaashauri ambayo itapisha maamzi hayo ndipo yatumwe wizarani.

“tumejaribu mara tatu kukaa wananchi tukishaamua maamzi yetu yanakwenda kwenye kata kisha halamahashauri, siku baraza la madiwani likikaa wanatafuta mihutasari inakosekana mara zote”anasema Mwenyekiti wa Hunyari

Malalamiko mengine wanaliyonayo nikukamtwa na kufungwa hovyo kwa wanafunzi wa shule mbalimbali zinazopakana na hifadhi hiyo wanapokuwa wamekwenda kunywesha maji Ng’ombe za wazazi wao.
Tayari wanafunzi wawili wamekamatwa na akari wa kampuni hiyo na kutupwa jela kwa kosa linaloonekana wazi kuwa la wazazi wao.

Wanafunzi hao ni Gujonju Said Gilabi (13 ambaye alimuwa mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mariwanda (B) wilayani Bunda Mwanafunzi mwingine wa Darasa la Sita Kihagazo Nyakile (14)aliyekuwa anasoma shule ya Msingi Kunzugu naye amejikuta akiacha masomo baada kufungwa kwa kosa kama hilo.

Akisimulia tukio hilo kwa masikitiko Kaimu Mwalimu kuu wa Shule hiyo Deus Mogasa anasema kuwa Nyakile ameshindwa kuendelea na masomo baada ya kuathirika kisaikolojia kutokana na kutupwa kwenye gereza la watu wazima Butimba Mkoani Mwanza.

‘‘Hii ilikuwa kumpa adhabu ndogo kama kuamsa na kumuonya tu lakini sasa walipomfunga miaka mitatu ni matatizo makubwa kwasababu humfundishi ila unazidisha chuki”alisema Mwalimu huyo kwa masikitiko.

Naye mzazi wa Mwanafunzi huyo Nyakire Kihagazo akizungumza na Tanzania Daima kijijini kwake Kunzugu alisema kwamba mtoto wake alikamatwa Disemba 30 Mwaka jana alipokuwa amepeleka ndama wake mtoni.

‘‘ Siku hiyo Mwanangu alikwenda kuchunga ndama na alipofika kwenye mto huo ambao unatutenganisha na hifadhi yeye akiwa nyuma na ndama mbele alipofika akakuta wamevuka akaenda kuwarudisha ndipo akakumbana na askari waliokuwa wamekamata wachungaji wengine watatu wakamuunganisha”alisema Mzee Nyakile.

‘‘Siku ya kesi ilipofika mshtakiwa namba moja alikuwa mwanangu kwa kuwa alikuwa mtoto aliposomewa Shtaka akakubali kosa akafungwa Miaka mitatu baadaye nikakata rufaa mahakama kuu Kanda ya Mwanza akachiwa kwa dhamana wakati kesi inaendelea”anasema Nyakire.

Mwanafunzi mwingine Gujonju Said Gilabi (13) anaendelea kutumikia kifungo cha Miaka 3 kwa kosa la kunywesha Ngombe wa Baba yake kwenye mto rubana unaotenganisha eneo ambalo mwekezaji kampuni ya Grumet Reserve.

Wakizungumza na Tanzania Daima kijijini Mariwanda kata ya Hunyari walimu wa Shule hiyo wanasema kwamba Mwanafunzi huyo Gilabi alikuwa ni miongoni mwa wanafunzi 10 bora waliokuwa wanatarajiwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka hu

Mwalimu kuu wa shule hiyo David Balijera, alisema kwamba mwanafunzi huyo ambaye alikuwa na uwezo mkubwa darasa ameharibiwa maisha kwa kosa ambalo kimsingi limekuwa likilipiwa faini ya shilingi 50,000.

“alipokuja hapa Waziri Shamsa Mwangunga baada ya kupata taarifa hizo alinuliza mimi kama mwalimu ili nidhibitishe nikamweleza ukweli lakini si kuona anafanya jitihada kubwa za kumtoa huyo mototo”alisema Baljera

walimu wengine waliozungumza na Tanzania Daima hapo walisema kwamba suala la kufungwa mwanafunzi huyo limetokana na uwelewa mdogo wa wananchi eneo hilo kushindwa kudai haki zao kwasababu mwanafunzi huyo hakuwa anamiliki mifugo hiyo.


kaimu afisa mtendaji wa kijiji hicho ambaye ni Mwalimu kuu wa Shule ya Msingi Mariwanda A, Damian Wegina alisema kwamba amekuwa akishudia wanakijiji hao wakifikishwa ofisini kwake kwa ajili ya kulipishwa faini na Askari wa Mwekezaji huyo bila kuhoji haki zao

Mwanafunzi huyo ambaye alikuwa afanye mtihani wake Oktoba Mwaka jana kwa kutumia namba PS0/9011137/013 alikamatwa na askari wa kampuni ya Mwekezaji Grumet Game Reserve Fund au maarufu kama VIP siku ya jumapili Agosti 30 Mwaka huo alipokuwa amepeleka mifugo ya baba yake eneo ambalo linalindwa na kampuni hiyo na kesho yake akahukumiwa miaka mitano jela.

Mzazi wa mwanafunzi huyo Matobora Meshinya (59) alisema kwamba mara baada ya kupata taarifa za kukamatwa mwanaye huyo kesho yake alikwenda moja kwamo hadi polisi na kukuta mtoto amekwisha pelekwa katika mahakama ya wilaya ya Bunda.

“nilipofika mahakamani nikakuta mwanangu amekwisha hukumiwa miaka mitano bila hata kupatiwa muda wa kujitetea nilipojaribu kutafuta uwezekano wa kuachiwa kutoka gereza la Nyasura nikaambiwa kwamba mototo amekwisha pelekwa gereza la Tabora B ,wilayani Serengeti”anasema mzee huyo kwa masikitiko.

Diwani wa hunyari,Kiarata anasema kwamba“hii ni moja ya unyanyasaji tunaoupata kutoka kwa mwekezaji huyu na tumejaribu kulalamika kila mahali imeshindikana,kwanza hiyo mifugo haikuwa ya huyo mwanafunzi alitumwa na mzazi wake akamchungie ndio maana tunashangazwa na jinsi kesi ilivyoendeshwa”alisema Kiarata.

Hukumu hiyo imelaaniwa na wanaharakati wa hakielimu ikiwemo Tume ya haki za binadamu na utawala bora, ambao wamesema kwamba watoto hao kulingana na kosa pamoja na umri wao walipaswa kuchapwa,kuonywa au kulipiwa faini.

Tasisi ya Hakielimu imesema kwamba hukumu hii imedhibitisha kilio cha siku nyingi kinachotolewa na familia za wafugaji wakidai watoto w ao wamekuwa wakinyaswa na serikali bila kupewa haki sawa.

Baada ya kukusanya malalamiko hayo ambayo nafasi haitoshi kuandika kwa kila tukio nilimtafuta msemaji wa kampuni hiyo Shaban Madanga ambaye alisema kwamba hali hiyo inatokana na wakazi wa eneo hilo kushindwa kufuata sheria za hifadhi wakikumbana na sheria wanalalamika.

“hayo sio malalamiko sio kitu kipya sheria za wanyamapori zipo na wananchi wanazijua ila wamekuwa wakikaidi tu wanaamua kupeleka mifugo yao eneo lisiloruhusiwa kisheria”alisema Madanga na kukata simu.

Lakini wakati naandika haya nilipokea simu kutoka kwa Mwenyekiti wa Kihumbu Kipeta Thomas akisema kwamba askari hao wamewachapa risasi wananchi wawili June 12 Mwaka huu wakati wananchi hao wakiwa miongoni mwa watu waliokuwa wanafuatilia ng’ombe zao.

Thomas anasema kwamba askari hao walikamata Ngombe za wakazi kadhaa wa vijiji hivyo saa 9:30 zilipokuwa zimekwenda kunywa maji katika mto rubana na kuzipeleka kwenye mazizi yao.

“ilipofika saa mbili usiku wenye ng’ombe wakapiga yowe wananchi kutoka vijiji vya Kihumbu,Mariwanda wakajitokeza kuanza kufuata nyayo za mifugo hiyo tulipoingia mbugani askari hao wakajitokeza na kuanza kutufyatulia risasi nakuwajeruhi wawili”alisema Thomas

Mwenyekiti huyo aliwataja watu waliojeruhiwa kuwa ni Gahamu Msome Mkazi wa Mariwanda ambaye alijeruhiwa kifuani na Juma Thomas Mkazi wa Kihumbu aliyepigwa risasi ya mguuni na kukimbizwa katika hospitali teule ya DDH bunda.

Thomas alisema kwamba kutokana na tukio hilo wamemua kuishataki kampuni hiyo ambayo imekuwa ikiendeleza vitendo vya unyanyasaji katika eneo hilo huku viongozi wa wilaya wakilinyamazia .

“Kwasasa hatukubali inabidi tuishtaki kampuni hii tumechoka kunyanyaswa na tunaona kundelea kunyamaza tunaumia sisi wenyewe maana hata viongozi wa Wilaya wanaona lakini hawataki kutusaidia ndio maana wameshindwa kuwakamata wale askari”anasema.

Je wananchi wa Bunda na Serengeti wataondoka kwenye utumwa huo kama wenzao wa North Mara walivyofanikiwa? Kila mmoja anaowajibu wa kuwasaidia.
\

Sunday, June 7, 2009

ufisadi waitafuna Serengeti

Mkurugenzi akiri kupokea nyaraka feki



na Mwandishi wetu,Serengeti


MKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti (DED) Kimulika Garikunga amekiri kupokea malalamiko ya wakazi wa Kata ya Issenye wakidai kuwa nyaraka za mihtasari ya vikao zilizowasilishwa kwake hatimaye kufikishwa kwenye baraza la madiwani kuonyesha kwamba wananchi wameafiki kutoa eneo lao kwa mwekezaji ni za kughushi.



Garikunga amesema kwamba katika madai ya wananchi hao wanasema kwamba hakuna mikutano ya hadhara iliyoitishwa na viongozi wa vijiji kama taratibu zinavyosema ili kupata kibali cha wananchi kutoa eneo la kuipatia kampuni ya Serengeti Holding Estate ambayo inataka eneo lenye ukubwa wa hekta 5000.



Baada ya kupokea malalamiko hayo Garikunga amesema kwamba ofisi yake imeamua kuchukua hatua za kuchunguza nakufuatilia madai ya wakazi hao ambao wameyawasilisha kwa niaba ya wenzao ili kubaini kama ni ya kweli kwamba hakuna mikutano ya wananchi iliyokaa nakuandaai nyaraka hizo.



“baada ya ofisi yangu kupokea malalamiko hayo imeanza kufanya uchunguzi kubaini kama viongozi wa kata za Natta na Issenye waliwasilisha kwangu nyaraka za kughushi kuonyesha kwamba wananchi wamekaa nakuafiki kutoa maeneo yao kwa kampuni hiyo”alisema Garikunga



Mkurugenzi huyo amesema kwamba awali diwani wa kata ya Issenye Chrismas Chabanga alimweleza kuwa taratibu zote zilizingatiwa ikiwemo kuitisha mikutano ya hadhara kwa wananchi wa Ihalala, Nyiberekera, Singisi na Mtukel ambao walikubaliana kutoa eneo hilo kwa malipo ya Milioni tano kwa Mwaka.



Kufuatia kuibuka kwa mgogoro huo tayari ofisi ya Mkurugenzi imesema kwamba itamzuia Mkurugenzi wa kampuni hiyo Nyaga Mawalla kwenda kupima eneo kama alivyokuwa ameidhinishwa na baraza la madiwani hadi pale mgogoro utakapopatiwa ufumbuzi.



Kampuni hiyo ilikuwa imepewa kibali na baraza la madiwani ambalo lilikaa Mei 8 Mwaka huu kujadili maombi ya kampuni hiyo na katika kikao hicho madiwani walilipwa posho na kampuni baada ya kupewa shilingi milioni 28 kwa ajili ya kuandalia kikao hicho.



Katika hatua nyingine baada ya kuibuka kashfa hiyo vyama vya NCCR-Mageuzi na CCM vyenye uwakilishi wa viongozi katika eneo hilo vimetoa agizo la kuchunguzwa viongozi wake waliohusika kughushi nyaraka hizo kisha kuziwasilisha katika baraza la madiwani na yakapitishwa.



Akizungumza na wandishi wa habari katika Kata ya Issenye katibu wa NCCR-Mageuzi, Wilaya ya Serengeti Mangasa Mkira

Alisema kwamba amemwita Diwani wake Chabanga aeleze jinsi alivyoshiriki kughushi nyaraka hizo na kuwasilisha mihtasari inayoonyesha kwamba wananchi walishafanya mikutano na kuafiiana kutoa eneo kwa mwekezaji.



“nimemwandikia diwani wangu afike ofisi ya wilaya ili aeleze jinsi alivyoshiriki kupitisha suala ambalo ni kinyume na taratibu za sheria ikibainika kwamba alifanya hivyo kwa maslahi ya binafsi ili kuchafua chama tutamvua uanachama wake ili kulinda heshima ya chama” alisema Mkira.



Naye Mwenyekiti wa CCM tawi la Ihalala Masoud Shashota alisema kwamba tayari wamepokea agizo kutoka wilayani wakitakiwa kuwaita na kuwahoji viongozi wote wa vijiji ambao wanatokana na Chama chake kufahamu ni jinsi gain walishiriki kuandaa nyaraka ambazo hazikushirikisha wananchi.



“sisi viongozi wa matawi tumepokea agizo kutoka CCM wilaya tukitakiwa kuwaita na kuwahoji viongozi wote wanaotajwa kuhusika na kuandaa nyaraka ambazo ni kinyume na taratibu za chama”alisema Shashota

MWEKEZAJI ALIPEWA ENEO LA MTU,

SERENGETI.

WAKATI Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti Kimulika Galikunga akitafakari kufuatilia pingamizi lililowekwa na wakazi wa kata za Issenye na Natta kuhusu eneo lao kupewa mwekezaji imebainika kuwa eneo hilo alikwisha pewa mkazi mmoja wa kijiji cha Nyiberekera toka mwaka 1986.

Huo ni mtihani wa pili kwa baraza la madiwani wa halmashauri hiyo baada ya mtihani wa kwanza kubainika kwamba hata mihtasari iliyotumiwa na baraza hilo kumpatia mwekezaji eneo lenye hekta 5000 ni ya kugushi kuonyesha kwamba wananchi wamekaa vikao wakakubali.

Hali hiyo imebainika huku bado kukiwa na mtafaruku mkubwa kutoka kwa jamii ikipinga maamzi ya halmashauri ya wilaya kujadili na kupitisha maombi ya mwekezaji huyo ya kuruhusiwa kupima eneo lao bila mchakato huo kuwashirikisha wananchi baada ya mihtasari hewa ilitumika kudanganya baraza.

Uchunguzi uliofanywa na waandishi wa habari umebaini kuwa katika eneo hilo alilopitishiwa mwekezaji wa kampuni ya Serengeti holding Estate limited inayoongozwa na mwanasheria Nyaga Mawalla kuna ekari 300 zinazomilikiwa kihalali na mkazi mmoja wa kijijini hapo Moremi Mwanangwa toka mwaka 1986.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo eneo hilo alipewa na serikali ya kijiji baada ya kufuata taratibu zote zinazotakiwa na kilichobaki sasa ni kulipia wapimaji na hakuna nyaraka zozote kutoka Serikali ya kijiji zinazotengua maamzi hayo yaliyofikiwa mwaka huo chini ya aliyekuwa mwenyekiti wa serikali ya kijiji Nyakanyenge Raphael.

Monangwa aliomba eneo hilo kwa ajili ya kilimo na ufugaji shughuli ambayo amekuwa akiifanya hadi hivi sasa licha ya uongozi wa kijiji hicho kuingia mengine ya kutoa eneo hilo kwa mwekezaji.

Mbali na Monangwa pia uchunguzi ulibaini kuwa eneo lingine ni makazi ya wananchi ambao wamekuwemo kwa muda mrefu hasa kundi la wafugaji ambao wanaitwa wahamiaji haramu ,huku katika shughuli za maendeleo wanashirikishwa kama wakazi halali wa kijiji hicho.

Diwani wa kata hiyo Chrismas Chabanga alikiri eneo hilo kukaliwa na wafugaji kwa muda mrefu,na kuwa wao wanawaona kama wahamiaji haramu kwa kuwa hawajapewa maeneo na serikali ya kijiji hicho.

Hata hivyo hakufafanua nia ya kutaka kumtumbukiza mwekezaji katika mgogoro wa mmiliki wa kwanza na hao wanaoishi eneo hilo ,ambao nje wanadai wahamiaji haramu na ndani wanawatambua kwa kuwa wanawashirikisha shughuli zote za maendeleo .

Baadhi ya wananchi waliwaambia waandishi wa habari kuwa kutokana na wakazi wanaoishi eneo hilo kutambuliwa kuwa wapo muda mrefu ,hata mkuu wa wilaya hiyo Edward Ole Lenga katika mkutano wake wa kuhusu wahamiaji haramu alishindwa kuwaondoa .

“Toka Oktoba mwaka jana alipokuja kufanya mkutano wake hapa mkuu wa wilaya aliagiza wahamiaji haramu waondoke.lakini hawa hawajaondoka kwa kuwa tayari wanatambulika”alisema Mkazi Mmoja
.

usafiri wa kivuko Kigamboni

video

Tuesday, June 2, 2009

Dk. Slaa: Makampuni hewa kikwazo madeni CIS

Na Sauli Giliard
Zikiwa zimepita siku kadhaa baada ya Mwakala wa kukusanya madeni sh. bilioni 200 mfuko wa madeni ya mfuko wa Commodity Import Support (CIS) kukiri kuwa hayalipiki, Katibu Mkuu wa Chama cha Maendeleo (Chadema) amesema kuwa hali hiyo inatokana na wakala huyo hatafanikiwa hadi pale suala hilo litakapofanywa la jinai.

Akizungumza na Tanzania Daima mwishoni mwa wiki, Dk. Slaa alisema kuwa suala hilo litafanikiwa pale ambapo serikali itaamua kuwatafuta wahusika walioandikisha makampuni hayo ambayo mengi yake ni hewa.

Kauli ya Kiongozi huyo imekuja pale ambapo Wakala wa Kukusanya madeni ya CIS, Msolopa Investment kukiri kuwa haitaweza kukusanya kiasi hicho cha fedha kutokana na wengi wa wakopaji ama kufariki au kufilisika.

“Wakala hawezi kukusanya madeni hayo. Hii inatokana na kuliweka suala hilo katika mfumo wa madai. Haiwezi kufikia lengo hadi pale itakapobalisha na kuwa jina,” alisema.

Kwa mujibu wa Dk. Slaa, hoja ya CIS haijulikani na baadhi ya wabunge kwa kuendelea kuona kuwa suala hilo lina sura ya madai na kuongeza kuwa ukweli wa suala hilo upo katika udanganyifu wa kuanzsha makampuni hewa na kujichotea fedha hizo.

“Sina ugomvi na waliokopa, hiyo ndiyo njia sahihi ya kuendelea, kuna tatizo hapa la kuunda makampuni hewa na kwenda kuchota fedha za umma. Kwa hali hiyo madeni hayo hayatalipika,” asisitiza.

Bila kumtaja jina, Dk. Slaa alisema kuwa kati ya makampuni 980 yaliyochukuwa fedha hizo, kuna kigogo alisajili kampuni moja yenye makampuni 35 hewa na kujipatia fedha hizo na kutokana na serikali kung’ang’ania kulipwa na makampuni yanayoonekana, fedha hizo zitabaki kuwa ni ndoto kupatikana.

“Hizi ni fedha nyingi kuliko hapa za EPA (Akaunti ya Madeni ya Nje) hata taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imetaka uchunguzi wa suala hilo kufanyiwa kazi.

“Mabilioni ya CIS yamepotea kupitia makampuni hewa, kinachotakiwa hapa ni uchunguzi na upelelezi na mashtaka ya jinai yafuate,” alisema kiongozi huyo.


Alisema washauri wa serikali wa masuala ya sheria wamekuwa wakilifumbia suala hilo macho na kuchukuliwa kama madia pekee, jambo alilolieleza kuwa halina mafanikio yoyote.

Mkurugenzi Mtendaji wa Msolopa Investment Company, Ibrahim Msolopa, ambaye ni wakala wa ukusanyaji wa madeni hayo alipoongea na gazeti hili alieleza kuwa kazi hiyo ya ukusanyaji madeni inakwenda kwa kusuasua kutokana na baadhi ya wahusika kutojulikana mahala walipo na shughuli wanazozifanya kwa sasa.

“Makampuni yenyewe hayaonekani, mengine yamefilisika ama wamiliki wake wamekwishafariki,” alisema mkurugenzi huyo katika mahojiano hayo na Tanzania Daima.

Msolopa alisema, kampuni yake inachukua muda mrefu kukusanya madeni hayo kwa kuwa inawabidi wafanye kwanza uchunguzi yalipo makampuni hayo, pamoja na anuani zao na kuongeza kuwa, kutopata msaada wa polisi, kumeongeza ugumu wa ukusanyaji wa madeni hayo ya zaidi ya miaka 20 iliyopita.

Kati ya makampuni 916 yanayodaiwa kukopa fedha hizo serikalini kwa lengo la kuagiza bidhaa nje ya nchi mara baada ya kutokea matatizo ya kifedha nchini, ndani ya kipindi cha miezi saba sasa, Msolopa Investments imeweza kuyafikia makampuni 450 tu, huku mengine yakiwa taabani na hayafanyi kazi na hayana uwezo wa kurejesha madeni hayo.

“Kwa kweli fedha zote kurudishwa haiwezekani kwani wengine wanalalamika kuwa hawakuchukua kabisa, hata waliokopa hawataki kulipa na wanafungua kesi kupinga kulipa madeni hayo.

“Kukosa msaada wa polisi, nako kumekuwa tatizo, endapo tungepata msaada, kasi ya ulipaji ingeongezeka,” alisema.

Hata hivyo, alikataa kuyataja majina ya kampuni na wamiliki wake waliokataa kurejesha madeni yao.

Halmashauri yakumbwa na Kashfa ya kughushi

*ni nyaraka za vijiji

Na Mchunguzi wetu
SERENGETI.

BARAZA la Madiwani halmashauri ya wilaya ya Serengeti limekumbwa na kashfa ya kupitisha maamzi ya kumpa mwekezaji eneo lenye makazi ya watu kwa kutumia nyaraka za kughushi.

Nyaraka hizo ambazo ziliwasilishwa katika ofisi ya mkurugenzi kama mihitasari ya vikao vya wananchi wa vijiji vinne vyenye eneo hilo zinaonyesha kwamba walikaa kuafikiana kutoa eneo hilo kwa mwekezaji.

Baada ya ofisi ya Mkurugenzi kupokea nyaraka hizo zilizowasilishwa na kamati ya maendeleo ya kata ya Issenye na Natta zilijadiliwa na kamati ya wataalam wa Ardhi, uchumi na Mazingira, uongozi, fedha na mipango hatimaye zikapelekwa kwenye baraza la madiwani ambao waliafikiana Mwekezaji apewe eneo lenye ukubwa wa ekari 5000.

Mwekezaji anayetaka eneo hilo ni kampuni ya Serengeti Holding Estate Ltd. inayongozwa na Nyaga Mawalla ambaye ni mwanasheria wa Kampuni ya Grumeti Reserve/Fund na katibu wa bodi ya Grumeti fund inayomiliki vitalu vya uwindaji vya Ikorongo na Grumeti.

Uchunguzi uliofanywa na waandishi wa habari katika vijiji vya Nyiberekera,Ihalala, Singisi na Mtukeli imebainika kwamba hakuna mikutano ya hadhara iliyokaa nakushirikisha wananchi katika kuamua jambo hilo kama ilivyodaiwa katika baraza la madiwani.

Aidha katika uchunguzi huo imebainika kwamba tangu kuanza kwa mchakato huo ngazi ya chini kampuni hiyo ilikuwa inagharimia posho za wajumbe katika vikao vilivyokuwa vinawashirikisha viongozi kujadili maombi ya mwekezaji.

Katika Kijiji cha Nyiberekera wananchi waliwaambia waandishi wa habari kwamba orodha ya majina iliyotumiwa na viongozi wao kuandaa mhitasari wa kijiji ilitokana na majina ya waombolezaji waliokuwa kenye msiba wa mwanamke mmoja kijiji hapo.

Mmoja wa wajumbe katika serikali ya kijiji hicho Moremi Monangwa alisema kwamba hoja hiyo ilipofikishwa katika vikao vya serikali ya kijiji ilishindikana mara mbili ikabidi ujanja utumike wa kughushi mhitasari wa wananchi.

“kijiji hiki kina vitongoji vitano lakini wametumia majina ya kitongoji kimoja waliokuwa wamekwenda kwenye msiba baada ya kujiandikisha kwenye daftari la waombolezaji ikafanywa ndio maazimio ya kijiji kukubali kutoa eneo kwa mwekezaji”alisema Monangwa

Mzee huyo anasema kwamba baada ya kushindana kwenye kikao cha serikali alitoka nje lakini baadaye alishangaa kuona jioni anapelekewa shilingi 8000 kama posho jambo ambalo halikuzoeleka katika vikao vingine.

Naye Tabu Salota anasema kwamba siku hiyo walikuwa wanatoka kwenye msiba wa Mke wa Magesa Kubena ambaye alifia bariadi na kuletwa kijijini hapo viongozi wa kijiji hicho wa kawasimamisha njiani nakuuwaleza wazo hilo.

“sisi wananchi tulikataa wazo hilo kwasababu eneo la kulima na kuchungia halitutoshi na kwasasa tu kuna mgogoro mkubwa kwa wafugaji na Mwekezaji Grumeti kabla hatujatoa eneo, je tukitoa itakuwaje,

lakini viongozi walikuwa wameandaa vijana ulipokuwa ukihoji wanakuzomea kwamba ni mchawi ikabidi kila mmoja atawanyike kivyake”alisema Salota

hata hivyo mwenyekiti wa kijiji hicho Juma Masubugu amefariki dunia siku chache baada ya maamzi hayo kupitishwa na baraza la madiwani ambapo sasa yamekuwa ni mwiba kwa viongozi waliobaki.

Katika kijiji cha Iharara wananachi wake wamesema kwamba hawajawahi kukaa kikao cha hadhara kwa ajili ya kupitisha maamzi ya kuipatia kampuni ya Serengeti Holding eneo la kuwekeza kwasababu hata wao haliwatoshi.

Mjumbe wa Serikali ya kijiji hicho Mlimi Song’ana aliwaambia wandishi wa habari kuwa anachofahamu yeye ni kwamba walikutana viongozi wa kijiji hicho ili kujadili eneo la kumpa mwekezaji baadaye wakapewa posho ya shilingi 7000 zilizotolewa na kampuni hiyo.

“ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kupokea posho kutoka kwenye kikao cha kijiji ,baadaye tulipoisha mkutano wa hadhara mmoja wa wa wanakijiji alisema ni vizuri kabla hatujaamua jambo lolote tukajua tukajua idadi ya wakazi na mifugo pamoja na ukubwa wa eneo letu ndipo tuone kama linatosha kumpa mwekezaji” anasema Song’ana


Anasema kwamba anachokumbuka kwenye mkutano huo waliazimia kwamba baada ya hapo uitishwe mkutano mwingine lakini amekuja kusikia kwamba mhitasari wa kijiji unaodai kuwa wamekubaliana umefikishwa kwenye baraza la madiwani wakati hakuna makubaliano yoyote..

Song’ana anasema mhitasari wa kijiji uliowasishwa kwenye kikao cha maendeleo ya kata kisha kwenye baraza la madiwani umeghushiwa kutokana na baadhi ya viongozi wa kijiji hicho kushawishiwa kwa pesa kwani wananchi hawajawahi kukaa nakuamua jambo hilo bado.


Aidha katika kijiji cha Singisi wananchi waliokuwa kwenye mnada wa Issenye waliposikia kwamba wanandishi habari wamefika hapo waliwakimbilia nakuwaeleza kwamba wako tayari kupigana kuliko kukubali maeneo yao kuuzwa kinyemela kwa mwekezaji.

Naye Olewa Dadela ambaye ni Mkazi wa Singisi alisema kwamba Kampuni hiyo ilikwenda kuomba eneo la kijiji chao wanalotumia kwa makazi na ufugaji walipomkatalia akaahidi kwamba atarejea tena kijiji hapo ingawa hajalejerea lakini tayari baraza la madiwani limeidhinisha apewe eneo hilo.

“huyu mwekezaji alikuja akatuomba eneo la hekari 5000 kwa ajili ya kulifanya kitalu cha uwindaji tukamkatalia akasema atarudi tena baadaye tunasikia kwenye vyombo vya habari amepewa eneo letu tumesikitishwa na kitendo hicho na sasa tunajiandaakwa vita atakapokanyaga hapa kijijini”anasema Dedela

Akizungumzia kashfa hiyo Diwani wa Kata ya Issenye (Nccr-Mageuzi) ambaye ni Mwenyekiti wa kikao cha maendeleo ya kata hiyo Chrismas Chabanga alisema kwamba wao walipokea mihtasari ya vijiji vyote kutoka kwa wenyeviti nakuijadili bila kujua kwamba imeghushiwa

Chabanga amekiri kusikia malalamiko ya wananchi ambapo amesema atawashauri wenyeviti wa vijiji hivyo kuitisha tena mikutano ya wananchi ili wapate maoni yao kama taratibu zilikiukwa.

“Wenyeviti waliwasilisha nyaraka za mikutano ya wananchi ,katika ODC ya kata na sisi tukalipwa posho ya 25000 na mwekezaji kwa ajili ya kumpitishia maombi yake ambayo tuliyatuma kwa mkurugenzi wa halmashauri kwa ajili ya kupitishwa na baraza hatukujua kwamba mihitasari zimeghushiwa”alisema Chibanga.

Hata hivyo wakati Diwani huyo akisema kwamba wataitisha tena mikutano hiyo tayari Mwekezaji huyo ameanza taratibu za kupima eneo hilo ili kuweza kujipatia hk.5000 ambazo atazitumia kwa shughuli za uwindaji huku akilipa halmashauri Milioni 10 kwa Mwaka.

Awali katika kikao hicho cha baraza la madiwani kilichoketi Mei 8
Mwaka huu Mbunge wa Serengeti, Dk.James Wanyancha aliwaonya madiwani kwamba wasidhubutu kutoa eneo hilo bila kupata maoni ya wananchi, hata hivyo baada ya kauli hiyo madiwani walimshambulia mbunge huyo wakimhoji alikuwa wapi siku zote mchakato ulipoanza.

Safari yangu Ndefu Mara-1

Mgodi waleta maafa ya mazingira

Na njemba ndinjemba

KATIKA safari yangu iliyochukua takribani mwezi mzima mkoani mara nimeshuhudia mambo mbalimbali ambayo kimsingi nikiamua kuyaandika kwa siku moja karatasi hazitatosha kuyakamilisha lakini kwa leo nafungua ukurasa kwa kuanza na uchimbaji wa dhahabu Mara.

Mkoa wa mara ni miongoni mwa Mikoa mingi hapa nchini ambayo imejaliwa kuwa na maliasili nyingi ambazo kama zingetumika ipasavyo sio tu ingekuwa na mchango mkubwa katika pato la taifa bali hata kwa wananchi wake wangekuwa juu kimaendeleo.

Ukweli huo unadhihirika kutokana na kuwepo shughuli nyingi za uchimbaji madini aina ya dhahabu katika wilaya mbili za mkoa huo ingawa wilaya zote za mkoa huo zina madini hayo.

Kwasasa wilaya ya Musoma ndio inaendeleza uchimbaji huo katika maeneo ya majita,majimoto na Buhemba ambapo wachimbaji wadogo wanaendelea na shughuli zao wakiwa na zana duni baada ya mgodi wa Buhemba kufungwa kutokana na kiwango kikubwa cha dhahabu iliyokuwa inatakiwa kupungua.

Lakini kwa wilaya Bunda hasa maeneo ya kandokando ya Mlima Balili ambapo inasadikiwa kuna madini hayo bado wachimbaji hawajaanza ingawaje wamewahi kudhubutu lakini kutokana na dhana zao butu walishindnwa kukabili mwamba wa mlima huo.

Katika wilaya ya Tarime ndipo inasadikiwa ilipo Ngome ya madini hayo ambapo katika utafiti uliofanywa na kampuni moja Mwaka 2001 ilibainika kwamba nusu ya ardhi hiyo imefunikiwa na madini hayo.

Kwasasa ni maeneo machache ndio uchimbaji huo unafanyika hasa katika vijiji vya Kenyamanyori,Kewamamba na eneo la Nyamongo ulipo mgodi mkubwa wa North Mara unaomilikiwa na Kampuni ya Barrick kutoka Kanada.

Kampuni hiyo imeingia eneo hilo baada ya kuuziwa mkataba na kampuni ya Afrika Mashariki Gold Mines (EAGM)ambayo iliondoka katika eneo hilo muda mfupi baada ya kuingia mikataba tata na viongozi wa vijiji hivyo.

inadaiwa kuwa mikataba hiyo ndio imekuwa chanzo cha vurugu kama tutakavyoona hapo mbele, wananchi wa hapo wakipinga uwekezaji wa kampuni ya Barrick na kuendelea kuhujumu miundombinu yake.

Afisa mawasiliano wa kampuni hiyo Edward Ibabila anasema kwamba kampuni hiyo imekuwa ikiendesha shughuli zake kwa hasara katika eneo hilo tafauti na maeneo mengine wanayofanyia kazi kama Bulyanhulu mkoani shinyanga.

Hata hivyo leo sihitaji kuelezea shughuli za uzalishaji wa kampuni hiyo bali nimeanza kuelezea ili kwa msomaji ambaye hafahamu hali hali ajenge picha ya kitu nachotaka kuelezea katika jambo hilo.


Katika mgodi huo ambao machimbo yake yamesambaa katika Vijijiji kadhaa eneo la nyamongo tarafa ya Ingwe imefahamika kwamba baadhi ya machimbo yake yanadhalisha sumu hatari ambayo ni hatari kwa mazingira aina ya Acid Rock Dranage (ARD)

Kufuatia hali hiyo maafa makubwa yanaweza kutokea kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa endapo Serikali haitachukua hatua za makusudi kukomesha Kemikali zenye sumu zinazotiririka kutoka kwenye mgodi wa North Mara na kuingia kwenye mto mara unaomwaga maji yake katika ziwa Victoria .

Tayari Kemikali hizo ambazo zimeonyesha maafa kwa viumbe wa eneo jirani zimesababisha hofu kwa wananchi wa tarafa ya Ingwe wilayani Tarime mkoani Mara ambao wameiomba Serikali kuchukua hatua za haraka kuokoa maisha ya watu na viumbe kutokana na mgodi wa North Mara kushindwa kuzuia hali hiyo kuendelea.

Hata hivyo kampuni ya Barrick wamejitetea kuwa wamekuwa wakifanya jitihada za kuzuia kusambaa kwa sumu hiyo kwa kuchimba mabwawa ya kuhifadhi maji yenye tindikali pamoja na kuweka kapeti ngumu chini ya mabwawa hayo lakini wananchi wamekuwa wakijipenyeza na kuiba hayo makepeti hivyo kuruhusu maji kutiririka.



Kemikali hiyo ambayo inatitirika kutoka katika mgodi wa Nyabigina na Kokona kuelekea mto tigita unaomwaga maji yake mto mara kuelekea ziwa Victoria ambalo linategemewa na wakazi wengi wa kanda ya ziwa imeonekana kuharibu vibaya mazingiria ya kijiji cha Kewanja ambapo nyasi , mimea pamoja na viumbe wa majini wamethibitika kufa.

hakuna kiumbe mwenye uhai aliyeonekana katika mto Tigita kutokana na ukali wa kemikali hiyo ambayo baadhi ya wananchi wa hapa walisema wameathirika kutokana na kugusana na maji hayo huku ikidaiwa kuwa ng’ombe zaidi ya tano wamekufa pamoja na samaki waliokuwa wanafugwa katika bwawa la jirani hapo.

Mmoja wa wakazi wa eneo hilo Omar Bina maarufu kama kidevu akilalamika samaki wake aliokuwa anawafuga katika bwawa lake kufa wote pamoja na viumbe wengine waliokuwepo hapo.



Alibainisha kuwa samaki hao amewafuga kwa muda mrefu toka mwaka 2003 na alikuwa amefikia hatua ya kuvuna ,na kuwa mwanzoni mwa mwezi huu alishangaa kukuta maji yamebadilika rangi na jirani yake nyasi zimekauka huku samaki wala wadudu hakuna hata mmoja ndani ya bwawa lake.

“hebu angalieni wenyewe ni jinsi maji haya yalivyo hatari hakuna hata kiumbe yoyote mwenye uhai anayeonekana hapa ,wamekufa wote pamoja na samaki niliokuwa nawafuga kwenye bwawa hili wala hakuna juhudi zozote zilizochukuliwa na serikali inagwa viongozi wanafika hapa wanaona hatari inayowanyemelea wakazi wanaotumia maji haya”alisema .



naye Paulo Magutu alisema kwamba tatizo kubwa linasababisha mazingira yanaendelea kuchafuka kutokana na sumu hiyo bila hatua zozote linatokana na viongozi wengi kutawaliwa na rushwa na kutowajibika na ukosefu wa maadili tu.



“ Tunajua kasi ya kushughulikia tatizo ni ndogo sana maana viongozi wakiwemo wataalam

wakifika wanafikia kwenye kampuni wanazungushwa na kujazwa maneno wanaondoka bila kukutana na wananchi ,hivyo sisi tunaona njia pekee hapa ni kuandamana kwa kuwa tatizo hili si leo nasi tunazidi kuzulika kila kukicha,”alisema kwa uchungu.

Hofu ya wananchi hao imeongezeka baada ya kuona viongozi kadhaa wa serikali waliofika eneo hilo walikishia kupokea maelezo tu kutoka kampuni na Barrik inayomiliki mgodi huo na kuishia kutoa agizo kwa kampuni hiyo kupima maji hayo na kutoa majibu kama sumu hiyo ni hatari kupitia kitengo chao cha mazingira .



Mtendaji wa kijiji cha Kewanja ulipo mgodi huo Julius Range alisema kwamba amepokea malalamiko ya Mzee Richard Masoya.aliyedai kupoteza ng’ombe wake baada ya kunywa maji hayo pamoja na watu wengine kudai kubabuka ng’ozi baada ya kuyaoga maji hayo na kuyatumia kwa matumizi mengine.



Range alisema kuwa watoto walioripotiwa kuathiriwa na maji hayo ni watoto wa mzee Masoya ambao aliwataja kuwa ni Julius Richard(11)anayesoma darasa la pili na mdogo wake Thomas Richard(6)darasa la awali shule ya msingi Nyabigena



“ni kweli yale maji ni hatari kwani hata nyie mmejionea wenyewe jinsi majani na miti ilivyokauka na hapa ofisini nimepokea malalamiko ya Mzee mmoja akidai kupoteza ng’ombe zake baada ya kunywa maji hayo nikamweleza aonane na afisa mifugo ili achukue vipimo na maelezo yake”alisema Mtendaji huyo.



Naye Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bogomba Rashidi alisema kwamba baada ya kuona hali hiyo aliwasiliana na kampuni ya Barick na Mei 11 Mwaka huu walikutana wakakubaliana kwamba kampuni hiyo itafute mbinu ya kuzuia kemikali hiyo isitiririke kuelekea mtoni kwani inaweza kuhatarisha maisha ya watumiaji wa maji ya mto huo unaomwaga maji mto mara ambao hutumiwa na viumbe wengi wakiwamo wanyamapori.



“sisi viongozi wa vijiji vinavyotumia maji ya mto huo tulikutana na uongozi wa kampuni hiyo tukakubaliana kwamba ivute maji hayo kutoka kwenye bwawa ambalo halijawekewa kampeti inayoyazua yasiteremke chini kisha wazibe bwawa lililokuwa na maji hayo kwa kuweka kapeti chini wakati wakiangalia taratibu zingine”alisema Mwenyekiti .



Alibainisha kuwa tatizo hilo limekuwepo kwa muda mrefu wananchi wakilalamika lakini limekuwa kubwa zaidi kipindi hiki na hata walipofika walishuhudia madhara ya moja kwa moja hali ambayo inaashiria kuwa asidi hiyo ni kali na kuomba ufanyike uchunguzi wa kina kubaini athari za baadaye na matokeo yawekwe wazi haraka .



Kwa upande wake Kampuni ya Barrick imekiri kwamba kemikali hiyo ni hatari kwa maisha na viumbe wote wanaotumia maji hayo ndio maana na wao wamekubali kukabiliana nayo kwa kuchukua hatua za dharura ikiwemo kuhamisha maji hayo kutoka kwenye bwawa ambalo walikuwa wameliweka kwa muda na kuyaweka katika mabwawa yenye kapeti ngumu chini ili kuzuia yasipenye ardhini.



Mkuu wa Kitengo cha mazingira mwandamizi wa mgodi huo Dolphinius Kabalege alisema kwamba tatizo hilo limetokana na baadhi ya watu kuingia kwenye mabwawa yanayohifadhi maji hayo na kuiba kapeti ambayo inazuia yasipenye chini na kuanza kusambaa ardhini kuelekea katika mto.



Pia alisema kwamba tatizo hilo limechangiwa na kifusi cha dhahabu walichokuwa wamerundika eneo hilo kwa muda baada ya mvua kunyesha hali imezidi kuwa mbaya kutokana na maji hayo kutiririka kuelekea mtoni hivyo kusababisha madhara ya kuunguza miti na mimea ,lakini alipinga kushuhudia wanyama wamekufa.



“nikiri kwamba kemikali hiyo ya asidi ni hatari kwasababu kuna kipindi watu waliwahi kupasua bomba linalosafirisha maji hayo kwenda mgodi wa pili, yalipomwagika kwenye dimbwi lenye samaki ndani ya muda mfupi walikufa wote lakini kwa sasa hatujashudia wanyama wamekufa kama wanavyodai wananchi”anasema Kabalege



Mwisho,inaendelea.



WAKAZI wanaoishi kando kando ya mto Mara unaomwaga maji yake katika ziwa Victoria wilayani Tarime wameonywa kutokula nyama ya mifugo wa aina yoyote atakayekufa eneo hilo wala kutumia maji ya mto huo kutokana na tindikali ya asidi inayotoka kwenye mgodi wa North Mara kusambaa eneo hilo .



Tahadhari hiyo imetolewa na Afisa Mifugo wa kata ya Matongo,tarafa ya Ingwe Paskal Masele baada ya kupokea malalamiko ya kufa Ng’ombe watano waliokunywa maji ya mto tigithe ambao unapokea chemichemi za maji ya tindikali na kuzimwaga katika mto Mara.



Masele alisema kwamba alipokea malalamiko hayo kutoka kwa mzee Richard Masoya mkazi wa kitongoji cha konsara ulipo mgodi huo ambapo baada ya kumtembelea mzee huyo alikuta wamekula nyama ile hali ambayo imemfanya kupiga marufuku wasile tena nyama kama akifa mnyama mwingine.



“baada ya kufika na kukuta watu wanakula nyama nimewazuia wasijaribu kula tena nyama watakapomuona mnyama mwingine wasijaribu tena kula wakati huo tukiendelea na uchunguzi na kwa suala la kutumia maji kila mtu sasa anayaona yalivyohatari ni vema wasiyatumie”alisema Masele



Kutokana na kula nyama zile tayari watoto wa yule mzee huyo wameonekana kuathirika na tindikali zile baada ya kuanza kubabuka mwili.



Masele alisema kwamba sumu inayotokana na miamba inayochimbwa ardhini na kampuni ya Barick sasa inaonekana kuwa hatari baada ya kuunguza miti na mimea yanapopita maji yenye tindikali yanapotoka mgodini kuelekea kwenye mto Tigithe.



Kutokana na kukatazwa nah al ilivyo katika mto huo akina mama wanadai kupata taabu zaidi kwa kufuata maji zaidi ya kilometa 3 hali ambayo inachangia kutumia muda mrefu kwa kazi hiyo na kuathiri shughuli zingine za maendeleo.



Monica Sariro (60)na Sirya Juliwa ambaye ni mjamzito walidai kuwa kitendo hicho cha kampuni hiyo kutiririsha maji yenye sumu katika chanzo chao cha maji kumewaathiri sana na kuwa sasa wanatembea umbali mrefu kutafuta maji ya matumizi mbalimbali.



Walidai kuwa pamoja na hayo hawajui hatima ya afya zao hasa watu wanaoishi kando kando ya eneo hilo ambalo limeathirika kwa nyazi na kilakitu kuungua kwa kuwa watoto wanakanyaga maji hayo,hivyo madhara huenda baadae yakawa makubwa zaidi.



Wandishi wa habari waliofika eneo hilo walishuhudia katika mto huo ukiwa mtupu bila viumbe wowote baada ya kudaiwa kuwa viumbe wote waliokuwa wanapatikana katika mto huo wamekufa wakiwemo samaki na vyura.



Kampuni ya Barick imekiri kwamba mto huo kwasasa maji yake hayafai kwa matumizi yoyote baada ya sumu aina ya Rock Acid Drainage (ARD)inayopatika katika miamba inayochimbwa kwenye mgodi wa Nyabigena kumwagika katika mto huo.



Afisa Mwandamizi wa kitengo cha Mazingira katika mgodi Dolphinus Kabalege alisema kwamba sumu hiyo inamadhara makubwa ndio maana hata nyasi na magugumaji yamekauka baada ya kupitiwa na maji yenye kemikali hiyo.



Hata hivyo Kabalege hakuweza kubainisha kwa upande wa binadamu inaweza kuwadhuru kwa namna gani ingawa alisema kwamba ameshudia samaki waliokuwa kwenye dimbwi eneo ili wakiwa wamekufa baada ya sumu hiyo kuingia hapo.



Chanzo na kutiririka kwa sumu hiyo kimebainika kwamba ni baada ya Barick kukaidi agizo la kuweka kapeti chini ya bwawa waliokuwa wamechimba kuhifadhi maji hayo huku wakidai kwamba ni la muda bila kujua kwamba lilikuwa linaruhusu maji ya sumu kutiririka kuingia kwenye mto unaotumiwa na watu wengi.



Naye mwanasheria wa Mazingira katika shirika la LEAT ,Tundu Lisu akizungumza na wandishi wa habari kwa njia ya simu alisema kwamba kwa mjibu wa sheria ya mazingira na madini ya Mwaka 2004 mwekezaji anatakiwa kurudisha mazingira katika hali yake ya awali kulipa gharama kwa walioathiriwa na uzembe huo.



Lisu alisema kwamba kwa watu walioumia kutokana na kudhuria maji hayo baada ya kuyaoga au kunywa wanapaswa kulipwa fidia na kampuni hiyo huku akisisitiza kwamba kampuni inapaswa kushtakiwa kwani hilo ni kosa la jinai.



“Mamlaka zinahusika kama baraza la taifa la mazingira NEMC na wizara ya nishati na madini wanatakiwa wachukue hatua za kuishataki kampuni hiyo kwa kukiuka sheria za mazingira”alisema Lisu



Naye mratibu wa shirika linaloshughulika na kuhifadhi bonde la mto Mara (WWF) William Kasanga amethiitsha kwamba yale maji ni hatari kwa maisha ya viumbe kutokana na asid ya hiyo ambayo aliita Salphur na madhara yake ya moja kwa moja hawajayabaini kwani wamepeleka vipimo katika maabara ya Mwanza ambazo wanasubiri majibu wakato wowote.

Wednesday, April 8, 2009

HAPPY BIRTH DAY TO US & YOU

SIKU Mtoto Emanuel alipoadhimika Mwaka mmoja wa kuzaliwa katika ofisi ya Gazeti la Tanzania Daima
hapa wanaoonekana kushoto ni Mobini Sarya na aliyemshika mhusika mwenyewe ni Mama Ema MAPAMBANO ,wanaoshuhudia ni wandishi pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Freemedia LTD jijini Dar es Salaam.

Happy Birthday to you

Mtoto Emanuel
Sarya Mobini a.k.a MAPAMBANO siku alipoitembelea ofisi ya Tanzania Daima Aprili 5 Mwaka 2009, alipotimiza Mwaka Mwaka Mmoja.

Wednesday, April 1, 2009

PONGEZI, SHUKURANI

PONGEZI
LEO KATIKA FAMILIA YA SARYA AMEZALIWA MTOTO WA KIUME


Familya ya Sir Mobini Sarya inayofuraha kubwa kumpongeza first Born wao, anayetimiza Mwaka mmoja April 5 Mwaka huu siku ya Jumapili.

Sherehe za kuwasha mishumaa ya kumpongeza mtoto wao Sarya Emanuel Bin Mobini (Mapambano) zitafanyika katika Mtaa wa Posta, Mkwepu ndani ya NewsRoom ya Tanzania Daima.

Hafla hiyo inafanyika kuanzia muda wa asubuhi, wote wanaopenda kujumuika kumpongeza mtoto huyo mzaliwa wa kwanza mnakaribishwa.

…………………
Ahsanteni

mtandao huu unamtakiwa 'HAPPY BIRTHDAY njema na maisha yenye mafanikio tele.

Friday, February 27, 2009

Profesa Saffari: najuuta kuifahamu CUF

*asema wajumbe wa cuf wamemdhalalisha vya kutosha
*sasa anajiandaa kuchukua uamzi mzito

Na ripota wetu

“SISIKITI kushindwa kwangu lakini najutia uamzi wangu wa kugombea uongozi CUF, nimesikitishwa na kufedheheshwa jinsi wajumbe wa mkutano mkuu walivyo nidhalalisha kwa kunizomea na kuniuliza ,maswali ya kizushi kama waliokuwa wametumwa hakika watanikumba, kwani wamekosa fadhila na kusahahu mchango wangu kwao”

hiyo ilikuwa kauli ya masikitiko iliyotolewa na Profesa Abdalah Saffari akielezea hatua ya kushindwa kwake vibaya na mshindani wake Profesa Ibrahim Lipumba ambaye amefanikiwa kutetea nafasi hiyo tena ya Mwenyekiti.

Katika mahojiano yake mwishoni mwa wiki Prof.Saffari alisema kuwa kwa hakika alikuwa haijui CUF kwa undani alikuwa anakisikia chama hicho kwa nje tu sasa amekifahamu vema baada ya kujitosa kugombea nafasi ya Mwenyekiti na kuambulia kura sita kati ya 665 zilizopigwa na wajumbe wa mkutano mkuu.

Anasema kujitosa kwake kugombea nafasi hiyo hakukuwa kwa bahati mbaya bali alikuwa na lengo la kuleta mabadiliko makubwa kwenye chama hicho na kukikwamua kutoka hapo kilipo lakini anasikitika kwamba wajumbe wa CUF wanaulewa mdogo wa kuchambua mambo.

Akitolea mfano huo anasema kuwa amesikitishwa jinsi wajumbe hao walivyokuwa wakimuuliza maswali yaliyolenga kumdhalalisha ambayo yalioonekana dhahiri kuwa yaliandaliwa kwa ajili ya kumkoamoa.

“nilishangaa sana kusikia yale maswali, yaani nimetoa hotuba yangu nzuri ambayo nilitarajia wangeniuliza maswali kutokana na kile nilichokisema lakini kutokana na uelewa wao mdogo wakabaki wananiuliza maswali ambayo yalikuwa nje kabisa na mada”anasema Prof.Safari.

Anasema kuwa kama asingekuwa na elimu ya Diplomasia na mtaalam wa sheria asingevumilia yale maswali angeondoka kama wanavyofanya viongozi katika mikutano ya Umoja wa Mataifa (UN)lakini kutokana na uelewa wake aliweza kuhimili mizaha yote hadi mwisho.

Baada ya uchaguzi ule amebaini kuwa ni mtu asiyetakiwa CUF ingawa alikuwa hajalijuwa hilo hivi sasa anatafakari uamzi wa kuchukua kwa kushauriana na marafiki ambao ni wasomi wenzake.

Alipoulizwa kama anampango wa kurejea CCM alisema kuwa ingawa amebaini chama hicho tawala kina Demokrasia ya ndani lakini hawezi kurejea huko kutokana na matatizo yake yanayoshabiana na ya CUF.

“baada ya mwezi mmoja nitaisha mkutano katika uzinduzi wa kitabu changu kinachoitwa ‘haja ya kuwa na Tume ya uchaguzi’ katika mkutano huo nitaeleza kila kitu na hatima yangu kisiasa, lakini sijaona chama cha kujiunga kwasababu usipokikuta ni CCM B basi kitakuwa kinatafunwa na ukabila au udini”anasema

Msomi huyo ambaye ni gwiji wa sheria ambaye amewahi kufundisha vyuo vikuu hapa nchini ikiwemo chuo cha Diplomasia ameweka wazi kuwa uhusiano wake na CUF upo mashakani na sasa anatafakari kazi ya kufanya ikiwemo kuishi kwa kuandika vitabu ambavyo atakuwa anauza Afrika mashariki.


“siwezi kusema siasa basi lakini kwa kweli nimebaini kwamba msimamo wangu na wajumbe wa CUF ni tafauti kabisa tena ni afadhali nimeshindwa nisingeweza kufanyakazi na Katibu mkuu Malim Seif Sharif, katika yangu na yeye mmoja angelazimika kujiuzulu… inaonekana hata wale wapemba wanachuki na mimi wamemfanya Prof.Lipumba kuwa kibaraka wao, hivi sasa CUF ikiambiwa ni chama cha wapemba Lipumba atajiteteaje”anasema Prof.Saffari

Alibainisha kwamba kushindwa kwake hakukutokana na sifa bali wajumbe waliandaliwa hasa wa kutoka zanzbar ili wamzomee na kumdhalisha kabisa wakionyesha kuwa ni mtu asiyetakiwa ndani ya chama hicho bila kuwa yeye alipoteza ajira yake serikalini kwa ajili ya kukitetea chama.

Prof.Safari ambaye naye ni miongoni mwa wahanga walioachishwa kazi serikalini katika mazingira ya kutatanisha
baada ya kubainisha nia yake ya kuunga mkono Chama hicho katika masuala ya kisheria anasema kuwa baba yake mzazi alifariki baada ya kusikia amefukuzwa kazi.

Akiwa Ofisi kwake anapojishughulisha na utunzi wa vitabu vya Riwaya na Sheria huku akisubiri kutoa uamzi wake kisiasa anasema kama ni masuala ya siasa ataangalia watu wenye msimamo kama wa kwake sio cuf tena chama ambacho kimebadili itikadi yake ya utajirisho na kugeukia sera za Liberal.

“ kwasasa namalizia kesi zilizobaki mahakamani ikibidi nitaziuza zingine ili niachane na masuala hayo niangalie mambo mengine ya kufanya lakini nimeamini kwamba msimamo wangu nitafauti kabisa na CUF”anasisitiza Prof.Saffari

Hata hivyo anasema kwamba hakujua kazi kubwa iliyokuwa mbele yake ili kupata Uongozi kwenye Chama hicho kikuu cha upinzani, “sikuwahi kujua kwa undani chama hiki sasa nimekifahamu vema ni bora nimegombea ningebaki nakisifu tu sasa ninaweza kukielewa”anasema

Anabainisha kwamba hakutarajia mjumbe kama kiongozi wa Kambi ya upinzani bungeni Hamad Rashid kutumia nafasi ya kuuliza maswali kumkandamiza kwamba alikataa kukisaidia chama hicho kusimamia kesi ya kupinga uchaguzi wa ubunge afrika Mashariki wakati amekisaidia chama hicho kwa muda mrefu bila kulipwa chochote.

Anasema ingawa Viongozi wa CUF bado wanashikilia msimamo kuwa watashiriki uchaguzi katika mazingira yoyote yale tafauti na walivyokuwa wakishikiria awali kwamba wanataka tume huru, yeye anabaki na msimamo wake kuwa hawawezi kuing’oa CCM katika tume hii ya uchaguzi ndio maana ameandika kitabu haja ya kuwa na tume huru ya uchaguzi.

“nimmejaribu kuwashaauri wenzangu wasishiriki uchaguzi wowote hadi Tume huru ya auchaguzi iundwe sambamba na Katiba ya jamhuri ili wawe kuiondoa CCM madarakani kiurahisi lakini hawanielewi, Tunduru wameshiriki,

Kiteto nako wameunga mkono CHADEMA pote wameambulia patupu na sasa ni huko tarime, nawambia huwezi ukashinda kwa sababu Kwenye uchaguzi CCM Ndio majaji na Uchaguzi ndio kesi unategemea nini?anasema Prof.Saffari alipofanya mahojiano na gazeti siku chache kabla hajaingia haingia kwenye uchaguzi

Anamaliza kwa kusema yeye hakugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CUF ili apate Ruzuku, alichotaka ni kukiunganisha chama kiwe na umoja tafauti na kinapoonekana sasa kama cha wapemba lakini Wajumbe wameshindwa kuona umhimu wake , sasa anasubiri kuwaita Viongozi wa upinzani siku ya uzinduzi wa kitabu chake awaeleze udhaifu wao.

Profesa safari alikuwa mkurugenzi wa masomo na mipango katika chuo kikuu cha Diplomasia Kurasini hadi alipoachishwa kwa sababu anazosema ni za kisiasa ,amezaliwa June 3 Mwaka 1951 ni mwislamu aliye na wake na watoto wawili.

Alimaliza elimu ya Sekondari Mwaka 1969 na kidato cha sita Mwaka 1972 kabla ya kujiunga na chuo kikuu cha M
limani Mwaka 1979 akichukua shahada na kisha shahada ya juu ya Sheria Mwaka 1985 katika chuo hicho.

Baadaye mwaka 1995 alikwenda kusoma uingereza chuo cha Sussex akizama zaidi kwenye sheria na kutunukiwa heshima ya Sheria Mwaka 2000 alipopewa Uprofesa.

Amewahi kushika nafasi mbalimbali ikiwemo kufanyakazi mahakama kuu kuanzia 1987 kama wakili hadi leo, amewahi kuajiliwa kama mtafiti msaidizi katika tasisi yaa uchunguzi wa Kiswahili 1972 hadi 1974 na kuwa mhariri wa nyumba ya uchapaji (TPH)1974 hadi1976 ,mwanasheria wa Serikali katika wizara ya sheria 1979 hadi 1986.

Mwaka 1987 alikuwa afisa mtafiti wa kituo cha uhusiano wa nje ,1988 hadi 1991 alikuwa mhadhili wa sheria baadaye Mwalimu mkuu wa Sheria hadi anaondoka pia Mwaka 2000 alikuwa mtaaluma mwandamizi wa sheria katika kituo cha uhusiano wa mambo ya nje.

Mawasiliano .mobinsons@yahoo.com

Thursday, February 12, 2009

MAFISADI WATINGA KWENYE TAALMA YA HABARI

Huu nao ni ufisadi, waandishi tukatae

Na kamanda wetu

NAWEZA kusema kuwa yamezuka makundi mengine ya kifisadi yanaloendeshwa na baadhi ya wajanja wachache wanaojulikana kama ‘makanjanja’ wa habari, yaani watu wanaojiita Waandishi wa Habari lakini hawana vyombo maalumu vya kufanyia kazi zao, ambao hivi sasa wamegeuza wanahabari halali kuwa vitega uchumi vyao .
Makundi hayo yanayoundwa na vijana wa kijiweni maarufu kama ‘vijana wa MAELEZO’ yamekuwa yakitumia majina ya kampuni za watu wengine kwa kuyabadilisha herufi kidogo na wao kuzitumia kuandaa semina za uongo kwa waandishi ili mradi wapate pesa kutoka kwa wafadhili ambazo hugawana bila jasho.
Moja ya njia wazitumiazo ni kuandaa fomu ambazo huzipitisha kwa waandishi wakiwataka wajiandikishe kwa ajili ya semina maalum ya waandishi wajanja, biashara au mambo ya dini; baada ya waandishi kujiandikisha hutumia majina yale kuwarubuni wafadhili mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara maarufu jijini Dar es Salaam ili wachangie semina hiyo muhimu kwa wanahabari.
Kundi hilo hudai kuwa katika semina hiyo kuna watu wataalam wameitwa kwa ajili ya kutoa elimu kwa wandishi hivyo wanahitaji kulipwa pamoja na nauli, posho na chakula; fedha ambazo hudai kuwa zinalipwa kwa wandishi kama posho ya kutwa ikiwemo chakula huku wakiwa na idadi yao inayoweza kuwa hata 100 kumbe ni wizi mtupu!
Makampuni ya biashara kama ya taasisi za fedha na wafanyabiashara huona kuwa hiyo ni njia moja ya kujitangaza kwa urahisi hivyo hujitokeza kwa haraka na kutoa michango yao ambayo wajanja hao huichukua na kuandaa semina ya uongo na ukweli ili mradi watimize lengo lao la utapeli!
Maajabu zaidi huanza kuonekana siku ya semina kwani mara wanapofika kwenye ukumbi wa semina vijana hao hufanya ujanja ujanja wa kusogeza muda ili siku imalizike bila hata kuwaleta wakufunzi wa semina hiyo, huku wakitumia muda mwingi kutafakari namna watakavyogawana dau hilo.
Moja ya semina hizo zilifanyika wiki iliyopita jijini Dar es Salaam, ambapo waandishi waliwekewa tangazo katika ukumbi wa Idara ya habari (MAELEZO), wakijulishwa kuwa kuna semina ya waandishi wa habari za biashara hivyo waandishi wote wanaotaka kujifuza masuala ya uchumi wafike hapo.
Siku ilipotimia wandishi walipofika wakakuta matangazo ya taasisi mbalimbali za fedha yametawala ukumbini hapo; wakaketi kusubiri wataalamu wajitokeze kuwafundisha masuala ya biashara na uchumi kama lengo la semina lilivyokuwa linasema.
Lakini hadi saa 12 jioni semina inafungwa, hakuna mtaalamu yeyote aliyejitokeza hapo wala hakuna mafunzo yaliyofanyika zaidi ya kuwapa nafasi baadhi ya wadhamini kujinadi namna wanavyotoa huduma kwenye kampuni zao hasa wenye mabenki na taasisi zingie za fedha.
Muda wa chakula ilipofika watu wakala na kurudi ndani; wakabadilishana mawazo hadi jioni akaingia mgeni rasmi ambaye ni mtu mkubwa tu anayeheshimika kwenye jamii. Aliingia bila kufahamu na inaelezwa kuwa hata yeye aliingizwa kingi kwa kuchangia semina hiyo.
Alifika kabla ya kuingia ukumbini akawekwa kando akasomeshwa jinsi semina ilivyokwenda vizuri! Baadaye akaingia ukumbini akafunga semina hiyo kwa kuwaahidi waandishi na hasa hilo kundi la makanjanja kuwa alikuwa amefurahishwa na mafunzo hayo kwa hiyo yupo tayari kwa kipindi kingine kuwalipa wakufunzi wa masuala ya biashara kama atajulishwa.
Baada ya kufungwa semina hiyo ukaanza utapeli usio na kificho kwani wanasemina walianza kuitwa mmoja mmoja na kusaini pesa kulingana na unavyofahamiana nao! Waliobaki wakaanza kupewa pesa kwenye bahasha wakifungua wanakuta noti ya shilingi 2000 huku wakiambiwa wasaini.
Wakishasaini sh 2000 baadaye zinaongezwa sifuri mbili na kubadilika kuwa laki mbili kila mtu! Kuwa kila mtu amelipwa 200,000! Kama huu si wizi wa mchana ni nini? Kwa kutambua mchezo huo mchafu baadhi ya waandishi waligoma kupokea pesa kwa maelezo kuwa ni mchezo mchafu kuwakalisha waandishi hadi jioni halafu unawapa sh 2000!
Hata hivyo juhudi zao za kupinga suala hilo hazikuzaa matunda kwani waandaaji wa mchezo huo waliendelea kujaza kiasi hicho katika majina ya waandishi wote waliofika ukumbini hapo na kuhalalisha kuwa kila mmoja amepewa fedha hizo.
Mara baada ya kufanikiwa kuzipata hizo pesa waliandaa sherehe nzito katika viwaja vya Karimjee ambapo walikunywa vinywaji na washirika wao wakijipongeza hadi usiku wa manane wakiwaacha waandishi wakilalama huku na kule wengine wakiapa kutoshiriki tena mchezo kama huo.
Hata hivyo wakati nikijiandaa kuandika makala hii nimepata taarifa kuwa vijana hao wanaandaa tena semina ya habari za dini na hivi sasa wameanza kupita katika taasisi na viongozi mbalimbali wa dini wakiwalaghai watoe pesa zitakazotumika kuwalipa wanasemina hiyo.
Tayari zimeonekana tena fomu kadhaa zikipitishwa katika eneo la MAELEZO wanapokutana waandishi wengi ili wajaze fomu hizo zitumike kwenda kutapeli pesa kwa watu kwa lengo la kuandaa semina batili.
Ni vizuri watu wawe waangalifu na mchezo huu kwani hakuna kampuni yoyote inayoratibu waandishi wa habari ; vipo vyama vinavyojulikana kama, Chama Cha Waandishi wa Habari za Mazingira (JET), Chama Cha Waandishi wa Habari za Ukimwi (AJAAT), Chama Cha Waandishi Wapigapicha (TPA) na Chama cha Kutetea Haki na Maslahi ya Waandishi (TCJ) ambacho kipo mbioni kusajiliwa.
Kwa hiyo ninazishauri benki na taasisi zingine za fedha kuwa hakuna kampuni wala chama kinachoitwa cha waandishi wa habari za biashara kama baadhi wa wajanja wachache wanavyotaka tuelewe; kwani kuna msemo usemao ‘unaweza kuwadang’anya watu wote lakini sio kwa wakati wote.

www.mobinday.blogspot.com. mobinsons@yahoo.com

Sunday, January 18, 2009

Ufisasdi ni chaka la waovu kujificha?

Na akiwlombe sahwaibu

TANGU neno au vita dhidi ya ufisadi imeibuka hapa nchini watu wameonekana kugawanyika katika makundi mawili ya wazi wakipingana kimtazamo wapo wanaojisifia kuwa ndio wapo mstari wa mbele kupambana na vita hiyo na wapo wanaoitwa kuwa ni mafisadi au watetezi wa ufisadi.

Kutokana na mgawanyiko huo baadhi ya watu wamekuwa wakitumia neno la ufisadi kuwaita wale ambao wanatofautiana nao kimtazamo ili mradi tu wamepingana nao.

Hali hiyo imekwenda hadi sasa kundi moja limefikia hatua ya kuwalazimisha watu wote wakubaliane wawe na mawazo ya pamoja hata kama wanajua ni kitu ambacho hakiwezikani binadamu wote wakawa na mtazamo mmoja.

Inapotokea watu wengine wakapinga kuwekwa wote kwenye kikapu kimoja wenzao waona ni maadui zao basi wanaamua kuwapachika neno hilo linaloonekana kama tusi dhidi ya upande usio kubaliana nao.

Lakini kibaya sasa kinachoonekana wazi kwamba vita ya ufisadi inatumika kwa manufaa ya kikundi fulani ni pale mtu au kiongozi abnapofanya kosa la wazi akiulizwa anaanza kujitetea kuwa hizo ni njama za mafisadi.

Yaani mtu anapiga na kujeruhi hata kutishia kuua hadharani kisha anageuka huyo huyo anasema mafisadi ndio wamesababisha afanye tukio hilo kwa lengo la kumnyamazisha katika juhudi zake za kupinga ufisadi.

Hali kadhalika tumezidi kushuhudia watu wakifanya makosa ya wazi tena ya jinai lakini wanakimbilia kuwatuhumu walalamikaji kuwa wapo mbele ya mafisadi.

Zamani mambo kama hayo tulizoa kuyaona wanasiasa wanayafanya kwamba mtu anabaka au kulawiti baadaye ikibainika anakimbilia kusema kuwa ni suala la kisiasa ambalo linakuzwa na wanasiasa kwa maslahi ya kisasa.

Hapo ndipo maswali yapoanza kuibuka kuwa je mwanasiasa yeye akifanya kosa anaonekana anaandamwa kisiasa wengine wakifanya wanashupaliwa sasa ndivyo wenzetu wanavyotaka tuamini katika vita hii ya ufisadi.

Wanataka kutufanya watanzania wote tuonekane kuwa sisi mazezeta tusiojua mchezo wao wa kufanya maovu halafu wanajificha kwenye chaka la ufisdi wakiulizwa wanasema ‘ni vita wapinga ufisadi na mafisadi’

Katika zama hizi za ukweli na uwajibikaji hatuwezi kukubali kutumia ,hisia zetu kuwahukumu wenzetu wakati sisi tukifikiri tutabaki salamaa kwa kutumia vita ya ufisadi kwa manufaa binafsi.

swali la masingi hapa ni lazima tujiulize kuwa ikisomwa albadili ya ‘ufisadi’ ni nani atakayepona katika nchi hii ambayo imepromoka kimadili na uzalendo maana kuna wengine wanataka kutufanya tuamiani kuwa ufisadi ni wa tabaka Fulani!.

Lakini ukweli ni kwamba tukiamua kuufungua masamiati huu wa ‘fisadi’ hapa nchini ni wachache waadilifu watakaopona hata viongozi wa dini watakwenda na huu mto maana wapo kandokando yake.

Wakati Fulani Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi , Yusuph Makamba lifanya ziara katika shule moja ya Sekondari mkoani pwani akiwa na msafara wake wanafunzi wa shule hiyo wakaanza kumzomea kuwa mafisadi hao.

lakini kabla mwalimu wao hajawaadhibu kwa fedeha hiyo Makamba akaomba watoto hao wampe kamusi awafafanulie maana ya fisadi ili wasije wakalitumia tena akasema.

“Hebu tungalie msamiati huo kwenye kamusi ya Kiswahili sanifu toleo la pili, iliyochapwa na chuo kikuu cha Oxford inasema kuwa; fisadi; ni mtu mbaya mtongozaji,mharibifu,mpotevu, mwasherati na guberi kwa maana ya Malaya,mfanya visa kiayari na mjanja”alimaliza Makamba.

Baada ya kuisoma Kamusi hiyo alianza kuwaonya watoto wale na kuwaleza kuwa yeye na msafara wake ni viongozi hawezi kuwa watongozaji,washerati na waharibifu mambo ambayo hata dini inazuia hivyo kuwazuia watoto hao wasitumie tena msamiati huo.

Watu waliokuwepo wanasema baada ya somo hilo wanafunzi hao wasekondari walionekana kushangazwa na maana ya jina hilo ambayo waliidaka tu kwa wanasiasa bila kuelewa maana yake wakaanza kuitumia.

Mfano huo unahusu makundi mengine ya wananchi ambao wamedaka msamiati huo nakuanza kuutumia kushambulia watu wengine kuwa ni mafisadi wakati katika maana halisi hata wao ni mafisadi.

Ufisadi sio lazima uibe pesa za benki kuu ya Tanzania (BOT) kwanza hatujaona maana hiyo, ufisadi unawahusu washerati wote pamoja na wale wanaozini na wake za watu au waume za watu je ni wangapi hawafany hivyo?

Watu wengi wanaoishi kwa mfumo wa kiujanja ujanja kwa kuwazulumu wafanyakazi wao wa ndani mshahara, kukataa kuwalipa kiasi kilichopangwa na serikali kuchelewesha mishahara yao nao ni mafisadi kwa maana hali ya jina lenyewe.

mabosi wote wanaowatongoza wafanyakazi wao, makazini kufanya vitendo vya kuwatishia wengine huo wote ni ufisadi ukiwemo hali ya mtu kuwa na tamaa ya kimwili kwa mjibu wa kamusi.

Kama ndio hivyo ni wangapi ambao sio mafisadi? Ni wangapi ambao kazini kwao hatumii ujanja unja kukukwepa kodi kuwadhulumu wafanyakazi kuwalipa kiasi kidogo ambacho hakiendani na kazi yenyewe huku wakibaki wanajitapa kupambana na ufisadi.

Tunaweza kupambana na ufisadi kwa kuanza kufagia nyumba zetu lakini vingenevyo ‘bongo’hii hakuna aliye msafi sote tu mafisadi kwa namna moja au nyingine tunapaswa kufanya kila jambo kujinasua kwenye tope hilo.

Wakati tukifanya hivyo tusitumie ufisadi kama kichaka cha kujikinga na maovu yetu kwamba tukiulizwa kwa yale tuliyoyafanya tunakimbilia kusema tunaandamwa kwa kuwa tupo mstari wa mbele kuopambana na ufisadi, kivipi wakati wote tupo gizani.

Friday, December 26, 2008

TUNAWATAKIA HERI YA MWAKA MPYA

siasa za nchi hii bwana ni fitna tupu hebu soma hapa http://www.mobiday.blogspot.com/

http://mobiday.blogspot.com/
walitaka Waitara agombee kama mboma?


hivi karibuni aliyekuwa mkuu wa majeshi Robert Mboma alitaka kugombea ubunge jimbo la mbeya jambo lililowatia hofu kubwa wapinzani

akili ya mtu nini wanasema heshima ya mtu ni utu soma- http://mobinig.blogspot.com/



NUKUU YA LEO

Mwandishi Robert Wieland katika kitabu chake, ‘Will Marriage Work in Today’s World’ anasema “wengi wametokea kuwa wenye huruma, wenye upendo na wakarimu katika jamii si kutokana na kuwiwa kwao bali kutokana na mateso ndani ya mioyo yao.
“Kutoa kwao pengine ni hatua ya kuziba ile ombwe iliyo ndani yao.”